Featured
Loading...

Watu sita wajeruhiwa na chui India

Watu sita wanauguza majeraha nchini India baada kushambuliwa wakijaribu kumdhibiti chui aliyekuwa ameingia kwenye shule moja.
Walishambuliwa wakijaribu kumdhibiti mnyama huyo.
Mwanasayansi na mfanyakazi wa idara ya msitu ni miongoni mwa watu wanaouguza majeraha baada ya kukabiliana na chui huyo kwa karibu saa 10 Jumapili.
chuiImage copyrightKashif Masood
Image captionMaafisa wa wanyamapori wanasema huenda chui huyo alitoka msitu ulio karibu
Chui huyo, aliyeingia shule ya Vibgyor, baadaye alidungwa sindano ya kumtuliza na kisha akaachiliwa arejee porini.
Sensa ya wanyama mwitu iliyofanywa majuzi nchini India inakadiria idadi ya chuo kuwa kati ya 12,000 na 14,000.
Chui huyo mwenye umri wa miaka minane alionekana akiingia kwenye shule hiyo katika eneo la Kundalahalli area.
Image copyrightReproducao
Kanda ya video iliyonaswa na kamera za usalama kwenye shule hiyo zilimuonyesha chui huyo akimshambulia mwanamume karibu na kidimbwi cha kuogelea.
Afisa wa wanyama pori Ravi Ralph ameambia mwandishi wa BBC Hindi Imran Qureshi kwamba chui huyo huenda alitoka kwenye msitu ulio karibu.
Baada ya kukamatwa, alipelekwa kwenye mbuga ya taifa.
Image copyrightKashif Masood
Chuo na wanyama wengine wamekuwa wakiingia maeneo ya makazi India.
Mwaka uliopita, chui mwingine aliyeingia kwenye kijiji kimoja jimbo la Rajasthan, kaskazini mashariki mwa India, alikwama baada ya kichwa chake kukwama kwenye chungu.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright 2025 UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top