Featured
Loading...

Wananchi wavunja miundombinu ya umwagiliaji shamba la mwekezaji TPC Kilimanjaro.


Wakulima wa mpunga katika skimu ya umwagiliaji Mawala kata ya Kahe wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamevamia na kuharibu miundombinu ya ugawaji maji kupeleka katika mashamba ya miwa ya  mwekezaji wa kiwanda cha sukari TPC.
Wakulima hao wamesema wamelazimika kufanya uharibifu huo na kuelekeza maji katika mfereji wa mashamba ya wakulima kwa madai ya mwekezaji huyo kukausha maji yote mferejini na kuelekeza kwenye mashamba ya miwa hali ambayo imesababisha kusababisha mpunga uliopandwa kukauka kwa kukosa maji.
 
Wamesema wanasikitishwa na hatua ya mwekezaji huyo kukiuka makubaliano ya kugawana maji hayo kwa wiki siku tatu badala yake anatumia mashine ya kuvuta maji yote mferejini na kueleleza kwenye mashamba ya miwa hali ambayo imesababisha mashamba ya mpunga kukauka kwa kukosa maji.
 
Diwani wa kata ya Kahe mashariki Bw. Rodrick Mmanyi amelazimika kufika katika eneo la tukio na kuwataka wakulima kuacha kufanya vurugu na kuahidi kushirikiana na viongozi wa umoja wa wakulima hao ili kufanya mazungumzo na uongozi wa kiwanda cha sukari TPC kumaliza mgogoro huo ambao unahatarisha amani.
 
Hata hivyo juhudi za kumpata afisa utawala wa kiwanda cha sukari TPC Japhary Ally kuzungumzia mgogoro huo hazikufanikiwa baada ya kusema yuko kwenye kikao ambapo kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Ramadhani Mungi amesema amepata taarifa hizo na kwamba yuko safarini atatoa taarifa hizo kesho.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top