Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesita kutangaza timu iliyopanda ligi kuu msimu ujao kutoka Kundi C, kutokana na utata wa matokeo ya michezo miwili ya kumalizia ligi hiyo iliyochezwa leo.
Wakati huo huo mara baada ya kuhitimishwa kwa michezo ya mwisho ya makundi ya ligi ya soka daraja la kwanza Tanzania bara na kuibuka utata wa matokeo ya michezo iliyohusisha timu zilizokuwa zikiwania nafasi ya kupanda daraja kwenda ligi kuu Tanzania bara shirikisho la soka nchini limefanya maamuzi yafuatayo kabla yakutangaza nani kapanda.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) halitatangaza timu iliyopanda Ligi Kuu msimu ujao kutoka Kundi C, mpaka itakapoamuliwa na vyombo husika vya TFF baada ya michezo ya kundi hilo kuchezwa leo jioni katika viwanja tofauti nchini.
TFF imefikia hatua hiyo ili kupata nafasi ya kupitia taarifa za michezo kati ya JKT Kanembwa v Geita Gold na Polisi Tabora v JKT Oljoro iliyochezwa leo jioni katika mikoa ya Kigoma na Tabora.
Taarifa za michezo hiyo kutoka kwa wasimamizi husika na vyanzo vingine vinakusanywa ili zifanyiwe kazi na vyombo husika vya TFF.
Katika michezo hiyo ya leo, Geita iliibuka na ushindi wa mabao 8 – 0 dhidi ya JKT Kanembwa, huku Polisi Tabora wakiibuka na ushindi wa mabao 7 – 0 dhidi ya JKT Oljoro.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment