Featured
Loading...

Magufuli: Sitaingilia mzozo Zanzibar

MzozoImage copyrightAFP
Image captionRais Magufuli ameshauri wasiokubaliana na hali waende mahakamani
Rais wa Tanzania John Magufuli amesema hataingilia mzozo wa kisiasa ambao unaendelea visiwani Zanzibar kuhusu uchaguzi.
Akiongea na Wazee wa Dar es Salaam, katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja katika vyombo vya habari, Dkt Magufuli amesema hakusudii kamwe kuingilia mzozo huo.
“Kuhusu Zanzibar, kama tume za uchaguzi nyingi duniani, haiwezi kuingiliwa na Rais yeyote ndiyo maana tume za uchaguzi huwa huru,” amesema Dkt Magufuli.
“Napenda kuheshimu sheria. Hiyo ZEC ina uhuru wa kuamua mambo yake lakini kama kuna tafsiri mbaya, waende mahakamani, mahakama ziko pale halafu unamwambia Magufuli ingilia.
Jukumu langu kama amiri jeshi mkuu ni kuhakikisha amani ya Zanzibar inaimarika, yeyote atakaeleta fyokofyko ajue vyombo vya usalama vipo."
Chama cha Wananchi (CUF) mwezi uliopita kilikuwa kimetoa wito kwa kiongozi huyo wa jamhuri ya muungano kuingilia kati.
Mzozo visiwani humo unatokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 20 Oktoba mwaka jana.
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza kwamba uchaguzi utarudiwa 20 Machi, hatua iliyopigwa na viongozi wa CUF ambao wamesema watasusia.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top