Ray amesema kuwa, filamu hiyo itatoka kama ilivyopangwa licha ya tuhuma za Batuli, akijitetea kuwa, hawezi kushindwa kumlipa mtu mmoja na kufanikisha kuikamilisha kazi hiyo waliyoifanya miaka 3 iliyopita tayari kwa kuiingiza sokoni.
Ray pia akatolea ufafanuzi hisia zilizoanza kujengeka kuwa, wametengeneza ugomvi huo na Batuli ili kuipatia kiki kazi yao, kitu ambacho amekipinga kwa nguvu.
“ Sinema ya Tajiri Mfupi itatoka kama kawaida katika utaratibu wake jinsi ulivyopagwa, sababau hakuna msanii yoyote aliyedhulumiwa kama nimeweza kutengeneza sinema yote nikaimaliza bajeti yake ni shilingi ngapi nishidwe kulipa msanii mmoja? Kwahiyo yeye ajaribu tu kutengeneza discipline katika kazi, kwasababu hawa dada zetu discipline katika kazi hawana kabisa, sasa hili linatakiwa liwe fundisho kwa wasanii wengine wakike kwasababu hawa wana mambo mengine wanaweza kuyafanya mabayo sisi hatuwezi kuyafanya, nimeshaandika kwenye Instagram yangu kama amedhulumiwa kuna vyombo kama mahakama polisi aende kushitaki au kuna chama kinaitwa TAFF cha mambo ya sinema Tanzania hapa kinatambulika kisheria, Lakini Mimi Ninahakika Kuwa Ni Movies Ambayo Ipo Sahihi Na Inatoka Kama Ilivyotakiwa Kutoka”- Ray alimaliza kueleza.
MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment