Juma Nature ameyasema hayo katika kipindi cha PlanetBongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba anamkubali sana msanii huyo kutoka Nigeria, ambaye ameimba wimbo wake wa Nagode kwa lugha ya kiswahili.
“Nataka nimalize kabisa na Yemi Alade, yeye ni msanii ambaye anaweza sana Afrika, anajua muziki kinyama, nikikaa nyumbani na kusikiliza madude yake, huyu dem Alade sio mtu mzuri, ujanja wangu woote yule kiboko, sijapata contacts ila najua nitazipata”, alisema Juma Nature.
Juma Nature amesema pia mwanamke huyo anajua anachokifanya ndio sababu anafikiria kumshirikisha kwenye kazi zake.
Pamoja na hayo Juma Nature ameelezea sababu ya kutoa nyimbo za Inaniuma sana na sitaki Dem na kuwa na kisa kinachofanana, na kusema kwamba kisa hicho kilikuwa na ukweli kuhusu maisha yake, baada ya kuumizwa na mwanamke ambaye alimpenda na aliyetaka kumuoa.
“Sitaki demu na inaniuma sana zilifuatana kwa sababu zilimuhusu mtu mmoja ambaye nilitarajia kumuoa, ilikuwa ni mara ya kwanza kutendwa, ukitendwa utaandika madude kibao utamkumbuka Necha, na imewatengenezea njia wengine”, alisema JumaNature.
Pia Juma Nature amesema pamoja na sababu hiyo msanii inabidi uwe mbunifu na kuacha kuiga, hivyo hata akiamua kutungia kitabu kutokana na kisa cha wimbo huo, kitafanya vizuri.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment