Wananchi wa kijiji cha Kisaki tarafa ya Bwakira wilaya ya Morogoro vijijini wamemkataa mwenyekiti wa kijiji hicho Ismail Ng’anja mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na kuzingira ofisi ya kijiji na kutaka kuichoma moto wakishinikiza mwenyekiti huyo ajiuzuru kwa madai ya kujihusisha na vitendo vya kupokea pesa za wafugaji wavamizi kwa lengo la kuwapatia maeneo ya kuchungia mifugo.
Wakizungumza kwa jazba kwenye mkutano ulioitishwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Morogoro kwa lengo la kujadili chanzo cha vurugu zilizosababisha mwenyekiti huyo kupigwa na wananchi wake mnamo Januari 15 mwaka huu wakiwa kwenye mkutano mkuu wa kijiji wananchi hao wamesema hawawezi kuvumilia viongozi wasio waadilifu wanaosababisha migogoro kati ya wakulima na wafugaji na kutaka kamati hiyo iondoke naye vinginevyo wangeweza kumshushia kipigo.
Pamoja na katibu tawala wa wilaya ya Morogoro Bwana Alfredi Shayo kujaribu kusuruhisha mgogoro huo kwa kuwashauri wananchi hao kufuata taratibu za kumuondoa mwenyekiti huyo kwa kuitisha mkutano mkuu wa kijiji lakini jitihada hizo zimegongwa mwamba jambo ambalo limezua mzozo mkubwa baina ya kamati hiyo na wananchi.
Baada ya hali ya usalama wa mwenyekiti ismail kuwa tete huku wananchi wakizingira magari ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya mwenyekiti huyo ameamua kujitokeza na kutangaza kijiuzuru wadhifa wake na hapa anasema.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment