Featured
Loading...

Wafanyabiashara 4 wakiwemo 3 raia wa Kenya wamekamata kwa uharibifu wa misitu Tanga.

Wafanyabishara wanne wakiwemo watatu raia wa Kenya wametiwa mbaroni na jeshi la polisi baada ya kukutwa na shehena ya magunia ya mkaa, na nguzo ambazo miti yake imevunwa kinyume cha sheria katika misitu ya hifadhi wilayani Mkinga kwa ajili ya kusafirishwa falme za kiarabu kupitia bandari ya Mombasa.
Hatua hiyo inafuatia operesheni maalum iliyofanywa kwa pamoja na jeshi la wananchi (JWTZ), jeshi la polisi na askari wa hifadhi ya taifa (TANAPA) kufuatia raia wema kusaidia kutoa taarifa kuwa umebainika kuwepo kwa mtandao mkubwa wa kuvuna misitu ya hifadhi kisha kusafirisha bidhaa zake katika falme za kiarabu kupitia nchini Kenya.
 
Akifafanua kuhusu operesheni hiyo, meneja wa misitu wilayani Mkinga Bwana Frank Chambo amesema kundi la mtandao huo unaojihusisha na uvunaji wa nyara za serikali kutoka nchini Kenya linalodaiwa kuwa na watu zaidi ya 200 katika msitu wa hifadhi wa Mwakijembe ni kubwa hivyo inahitajika nguvu ya ziada kuweza kukabiliana na kundi hilo ambalo linakiuka makubaliano baina ya nchi hizo mbili ya kuheshimu raslimali za mwenzake.
 
Hata hivyo mmoja kati ya viongozi wanaongoza mtandao huo nchini Kenya aliyefika wilayani Mkinga kwa ajili kujua mustakabali wa wenzao kutiwa mbaroni, Tito Mayui amesema wamekuwa wakiwatumia baadhi ya viongozi wa serikali ngazi za vijiji na kata kwa kuwalipa fedha wakati wanapopitisha shehena za mkaa na vigogo wakidai kuwa walidhani kuwa fedha hizo wanazifikisha katika mamlaka husika lakini kumbe zinaishia mikononi mwao.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top