Featured
Loading...

MOJA KWA MOJA: Matokeo ya uchaguzi Uganda

10:37 Kiongozi wa waangalizi wa IGAD Yufnalis Okubo asema kwa maoni ya kundi lake la waangalizi, uchaguzi ulitimiza viwango vinavyohitajika kimataifa. Ahimiza walioshiriki kukubali matokeo. Awataka wasioridhika kutumia mifumo ya sheria kulalamika.
10:30 Kiongozi wa waangalizi wa IGAD Yufnalis Okubo anasema kulikuwa na changamoto katika kuandaa vituokwa upigaji kura pamoja na kufunguliwa kwa vituo. Asema pia waliona mabango ya kampeni katika baadhi ya vituo vya kupigia kura. Asema siku ya uchaguzi, baadhi ya wapiga kura walikosa majina yao vituoni. Wasiojua kusoma hawakusaidia vyema. Waliofaa kupaka watu wino baada ya kupiga kura katika baadhi ya maeneo hawakumakinika sana. Apendekeza vifaa vya kupigia kura viwe vikifikishwa mkesha wa siku ya kupiga kura, sawa na kuandaliwa kwa vituo.
10:25 Kiongozi wa waangalizi wa COMESA Ashraf Gamaal Rashed amesema Tume ya Uchaguzi inafaa kuwezeshwa zaidi ili kutekeleza majukumu yake vyema.
10:20 Waangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, COMESA na IGAD wanatoa taarifa zao kuhusu uchaguzi. Rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi amewapongeza wananchi wa Uganda kwa kujitokeza kwa wingi. Amesema uchaguzi ulifiofanyika wiki hii ulikuwa na ushindani mkubwa.
09:59 Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umekanusha taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa mitandaoni zikiashiria kwamba Marekani imewaagiza raia wake waondoke Uganda. Ubalozi huo umesema taarifa hizo ni za uongo.
08:44 Bw Kiggundu amesema matokeo mengine yanatarajiwa mwendo wa saa nne, lakini yanaweza yakatangazwa mapema iwapo yatakuwa tayari. Ametetea tume hiyo dhidi ya madai kwamba kura kutoka 'ngome za upinzani' hayajaripotiwa. Tume inatarajiwa kutangaza matokeo kamili kabla ya saa kumi alasiri kwa mujibu wa sheria.
08:38 Matokeo yaliyotangazwa sasa hivi ni kama ifuatavyo. Ni kutoka vituo 21,254 kutoka kwa vituo 28,010. Matokeo yaliyotangazwa yanajumuisha kura 7,822,737 ambazo ni sawa na asilimia 51,21 ya wapiga kura 15 milioni waliosajiliwa na tume hiyo. Kumbuka si wapiga kura wote waliosajiliwa ambao hufanikiwa kupiga kura.
Matokeo kwa sasa (Vituo 21,254 kati ya 28,010)
Abed Bwanika70,7080.95%
Amama Mbabazi112,0711.50%
Baryamureeba Venasius42,9310.58%
Benon Biraaro20,5530.28%
Kizza Besigye2,603,88034.94%
Joseph Mabirizi19,6610.26%
Maureen Kyalya32,7730.44%
Yoweri Museveni4,549,14861.05%
Chanzo: Tume ya Uchaguzi Uganda (EC)
08:33 Mwenyekiti wa EC Badru Kiggundu anaanza kutangaza matokeo ya karibuni zaidi.
08:32 Kwa sasa ni wakati wa maombi Namboole, kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya kwanza ya urais ya karibuni zaidi leo.
08:28 Katibu Mkuu wa chama tawala cha NRM Justine Kasule Lumumba amekuwa akiwahutubia wanahabari kutoka Bweyogerere
Museveni anaongoza. NRM inaongoza katika kura za urais na za ubunge na tunasubiri matokeo ya mwisho. Hata kule mawaziri wameshindwa, ni watu wa kawaida. Waganda waliamua nani anafaa kuwaongoza. Kwa NRM si habari njema, lakini ni lazima tukubali.
08:13 Waangalizi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuhutubia wanahabari kuhusu uchaguzi mkuu wa Uganda saa sita kasorobo.
08:10 Mwenyekiti wa EC Badru Kiggundu ameingia ukumbini kutangaza matokeo ya karibuni zaidi ya uchaguzi.
07:54 Tume ya taifa ya uchaguzi Uganda inatarajiwa kutoa matokeo mengine mwendo wa saa mbili asubuhi.
07: 52 Matokeo yaliyotangazwa kufikia sasa ni kama ifuatavyo:
Matokeo kwa sasa (Vituo 15,799 kati ya 28,010)
Abed Bwanika51,150
Amama Mbabazi88,900
Baryamureeba Venasius33,135
Benon Biraaro15,588
Kizza Besigye1,767,041
Joseph Mabirizi14,757
Maureen Kyalya24,536
Yoweri Museveni3,156,070
Chanzo: Tume ya Uchaguzi Uganda (EC)
07:50 (Saa za Afrika Mashariki) Hujambo! Twatumai umeamka salama. Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu uchaguzi mkuu wa Uganda. Matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi nchini Uganda yanaendelea kutangazwa, matokeo kamili yakitarajiwa kutolewa baadaye leo alasiri.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top