Featured
Loading...

Msichana kutoka China atamba mtihani wa taifa Tanzania

Congcong Wang
Image captionBi Congcong alisomea shule ya wasichana ya Feza
Msichana kutoka China ameibuka wa pili kwa ubora katika matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta).
Congcong Wang, 16, alifanyia mtihani wake shule ya upili ya wasichana ya Feza iliyoko eneo la Kinondoni, Dar es Salaam.
Congcong Wang
Image captionCongcong Wang (kushoto) akiwa na mamake
Bi Congcong, aliyepata alama B katika Kiswahili, anatoka jiji la Changchun katika mkoa wa Jilin nchini Uchina.
Ameambia wanahabari kwamba ameshangazwa sana na matokeo hayo.
Congcong
Image captionBi Congcong alipata B katika somo la Kiswahili
"Sijawahi kudhani ningekuwa mmoja wa wanaoongoza. Nimekuwa nikitia bidii masomoni lakini sikutarajia hili,” amenukuliwa na gazeti la The Citizen.
Alijiunga na shule za Feza mwaka 2006 akitokea China na akalazimika kujifunza Kiswahili na Kiingereza.
Mwanafunzi bora kitaifa alikuwa Butogwa Shija, 17, kutoka shule ya wasichana ya Canosa, Dar es Salaam.
Jumla ya wanafunzi 240,996 walifanya mtihani huo wa kitaifa Novemba mwaka jana.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top