Featured
Loading...

Watoto Wilayani Moshi walinajisiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja

Watoto wanne wa kike wenye umri wa miaka nane, wamebainika kubakwa na kunajisiwa kwa karibu mwaka mzima huku vijana wawili wanaowafanyia vitendo hivyo wakiwalipa Sh 500 kila mmoja.

Habari zinasema watoto hao wanaosoma darasa la tatu katika shule ya msingi ya Msaranga katika Manispaa ya Moshi, wamekuwa wakienda kufanyiwa vitendo asubuhi kabla ya kuingia darasani.

Uchunguzi wa madaktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa Kilimanjaro ya Mawenzi umethibitisha watoto hao kuingiliwa sehemu za siri na kunajisiwa na pia wameambukizwa magonjwa ya zinaa.

Watoto hao wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo kati ya saa 12:30 na saa 1:30 asubuhi na baadae hutakiwa kurudi saa 4:00 wakati wa mapumziko ili kuchukua Sh500 kama malipo ya kazi hiyo.

Tukio hilo ambalo limeibua hasira za wananchi, linafanana kwa kiasi na lile la mwanamuziki Nguza Viking “Babu Seya” na mwanae Jonson Nguza “Papii Kocha” wanaotumikia kifungo cha maisha jela.

Wanamuziki hao raia wa Congo walihukumiwa kifungo hicho mwaka 2004 kwa tuhuma za kubaka na kunajisi watoto 10 wenye umri wa miaka 6 na 8 wa shule ya msingi Mashujaa ya Jijini Dar Es Salaam.

Mzee Alex Massawe (sio jina lake halisi), mkazi wa Msaranga mjini Moshi, alisema kuwa Jumatano iliyopita, alishuku mwenendo usio wa kawaida wa mjukuu wake mwenye umri wa miaka nane.

Habari hii iliandikwa na gazeti la Mwananchi

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top