Featured
Loading...

Mshukiwa wa mashambulio ya Brussels ‘atambuliwa’

Laachraoui
Image captionLaachraoui alikuwa akitafutwa kuhusiana na mashambulio ya Paris
Mshukiwa aliyekuwa akisakwa sana kuhusiana na mashambulio ya Brussels ametambuliwa na maafisa wa usalama, vyombo vya habari Ubelgiji vimeripoti.
Baadhi ya vyombo vya habari limetaja jina lake kuwa Najim Laachraoui.
Wadadisi wanasema Laachraoui anaaminika kuwa mtaalamu wa kuunda mabomu.
Alionekana kwenye picha ya kamera za usalama uwanja wa ndege akiwa pamoja na washukiwa wawili ambao inadaiwa walijilipua wakati uwanja wa ndege wa Zaventem.
Alikuwa tayari anatafutwa na polisi kuhusiana na mashambulio ya Paris mwaka jana.
Ripoti za kukamatwa kwake bado hazijathibitishwa na maafisa wa usalama.
Taarifa za awali zilikuwa zimewatambua washukiwa walioonekana naye kwenye uwanja wa ndege kuwa ndugu wawili, Brahim na Khalid El Bakraoui.
Watu 34 walifariki na zaidi ya 250 kujeruhiwa kwenye mashambulio mawili yaliyotokea katika uwanja huo wa ndege wa Zaventem na kituo cha treni cha Maelbeek.
Kundi linalojiita Islamic State limedai kutekeleza mashambulio hayo.
Bendera zinapepea nusu mlingoti nchini Ubelgiji. Taifa hilo limetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top