Featured
Loading...

Wimbo wa Ney wa Mitego haufai katika jamii- BASATA


BASATA imetoa kauli hiyo kupitia Katibu mkuu mtendaji wa baraza hilo Godfrey Lebejo, alipokuwa akiongea katika kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba anaamini hata kwenye media wimbo huo hautapigwa.
“Ni wimbo ambao haufai na ni msanii ambaye I dont know hata unashindwa kumpima ana akli ya namna gani, au kwa nini ameamua kufanya hivyo, lakini watu kama hao kwenye jamii wapo, ni kazi ambayo haifai katika jamii kwa hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zake, kitu ambacho hakifai kwenye jamii sio mpaka litolewe tamko kwamba wimbo umefungiwa, ni wimbo ambao haufai hata wanajamii wameona haufai, nadhani mtu mwenye akili timamu kiujumla anajua, najua kwenye media hauwezi kupigwa”, alisema Godfrey.
Katibu huyo wa BASATA amesema kinachotakiwa kwa Ney ni kujitambua kama yeye ni kioo cha jamii, na kwa kufanya vitendo kama hivyo si sahihi kwake kwani jamii inamtazama yeye.
“Anachofanya afikirie yeye ni nani na ana nafasi gani kwenye jamii, kwa sababu mtu anayefanya namna hii asidhani kama anamdhalilisha mtu, anajidhalilisha yeye mwenyewe kwa sababu mtu yeyote ambaye anatoa lugha chafu, anafanya vitendo vya aibu, asidhani kama anamdhalilisha mtu, kwa hiyo yeye mwenyewe ni kama hayawani fulani tu”, alisema Godfrey Lebejo.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top