Featured
Loading...

Watu watano wa familia moja wanusurika kifo mkoani Morogoro.

Watu watano wa familia moja wakiwemo watoto watatu katika mtaa wa Sume kata ya Mwembesongo manispaa ya Morogoro wamenusurika kifo baada ya nyumba wanayoishi kuangukiwa na ukuta wa uzio wa kituo cha mafuta cha total usiku wakiwa wamelala.
ITV imefika katika eneo hilo na kushuhudia nyumba hiyo ikiwa imebomoka kabisa upande wa nyuma ambapo majeruhi wa tukio hilo wameeleza jinsi lilivyotokea huku wanafamilia wamelalamikia kulala nje kwa zaidi ya siku tatu na hawajui hatima yao kutokana na mmiliki wa kituo hichi kushindwa kuwasaidia na kwamba kabla ya ukuta huo kuanguka walitoa tarifa lakini hazikufaniwa kazi.
 
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa Sume Hamis Totoro amesema tukio hilo limetokea majira ya usiku ambapo majeruhi waliwahishwa hospitali ya rufaa ya mkoa Morogoro pamoja na hali zao kuendelea vizuri lakini mmoja wao ambaye ni mzee amehamishiwa katika hospitali ya Agakan jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
 
Kufuatia tukio hilo ITV imemtafuta mmiliki wa kituo hicho cha mafuta cha Total bila mafanikio baada ya simu yake kuita bila kupokelewa ingawa pia wafanyakazi wa kituo hicho wameshindwa kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari huku wakiwazuiya kupigapicha kituo hicho. 

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top