Featured
Loading...

Madereva daladala Mbeya wamegoma na kusababisha adha ya usafiri kwa abiria.

Wakazi wa jiji la Mbeya leo wamejikuta katika wakati mgumu kwa kukosa usafiri wa kuingia na kutoka katikati ya jiji baada ya madereva wa daladala zinazofanya safari zake kati ya Uyole na Stendi kuu kufanya mgomo ambao umeambatana na vurugu kubwa wakipinga njia wanazopita kwa madai kuwa ni mbovu, hali ambayo imesababisha jeshi la polisi kuingilia kati na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi.
Madereva wa daladala zinazofanya safari zake kati ya Uyole, Isyesye na Ituha uelekea maeneo ya Majengo na Stendi kuu jijini Mbeya leo wamefanya mgomo ambao umeambatana na vurugu kubwa wakipinga kupita kwenye barabara kadhaa ambazo wamepangiwa na Sumatra kwa madai kuwa barabara hizo ni mbovu na hazina vituo vya kupakia na kushusha abiria.
 
Kutokana na vurugu hizo jeshi la polisi limeamua kuingilia kati kwa kuwatawanya madereva hao kwa mabomu ya machozi na akizungumzia mgomo huo, kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, kamishna msadizi mwandamizi wa jeshi la polisi, Ahamed Msangi amewataka wakazi wa jiji la Mbeya kuwa watulivu akisema kuwa hakuna sababu za kufanya fujo kwa sababu malalamiko ya madereva hao ni jambo linazozingumzika huku akidai kuwa anaamini kikao cha dharura ambacho kimeitishwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Abaas Kandoro kikihusisha wadau wote wa usafirishaji kitatoa ufumbuzi wa tatizo hilo

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top