Zaidi ya watu mianne wa kijiji cha Themiyasimba wilaya ya Arumeru wameandamana hadi kwenye shamba la mwekezaji wakitaka kugawana sehemu ya shamba ilo kwa madai mwekezaji amepewa shamba la hekari elfu tatu lakini ameshindwa kuliendeleza na kuanza kuuuza kwa wawekezaji kutoka nje huku wananchi wakikosa ardhi ya kuweka huduma muhimu za kijamii hali iliyowalazimu viongozi wa kijiji na kata kuingilia kati kisha wananchi wakatoa wiki moja la sivyo watafanya maamuzi magumu.
ITV ilifika katika kijiji cha Themiyasimba na kushudia umati mkubwa wa wananchi waliyo zungumza kwa jazba wakisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuteseka kwa muda mrefu bila huduma za kijamii kama shule zahanati na kituo cha polisi huku wakizungukwa na mashamba makubwa yasiyo endelezwa na kuuzwa kwa wawekezaji kutoka nje ambao wengine uyauza tena na kuwakata wananchi wanunue hekari moja kwa shilingi milioni mbili huku wakitambua kwamba hawana uwezo huo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Themiyasimba Emanuel Wiliam alitumia muda mrefu kuwaomba wananchi kuacha kugawana shamba ilo kwakuwa ni kinyume cha sheria na kuwataka kuwa nasubira wakati wakifanya mawasiliano na uongozi wa juu.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Bwawani Lazaro Lukumay amesema kumekuwa na tabia ya wawekezaji kupewa mashamba makubwa na kushindwa kuyaendeleza kisha kuyauza na kuwakodisha wananchi kwa bei ya juu hivyo ameitaka serikali kuangalia upya umiliki wake ili kuepusha migogoro isiyo na tija.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment