Featured
Loading...

KUANZIA SASA MTAWASILIANA BAADA YA KUOMBA KIBALI! Na. Mtatiro J


Serikali imeweka masharti magumu sana kwa mabalozi wa nchi za kigeni na maafisa wao, mashirika ya kimataifa na wageni wote wa kimataifa walioko nchini Tanzania kuomba kibali kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania kabla ya kukutana na viongozi wa vyama vya siasa ama maofisa wa mashirika mbalimbali na pia imeweka masharti magumu kwa wahusika kusafiri na kuonana na mashirika ya binafsi na ya serikali au viongozi wa vyama vya siasa wa ngazi ya chini.
Kwamba leo kama Balozi wa Uingereza anataka kutembelea Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) au Chama Cha Wananchi (CUF) au Shule ya Sekondari (TUSIIME) lazima kwanza aiandikie wizara ya Mambo ya Nje akishapewa majibu na kuruhusiwa ndipo apange siku ya kwenda. Duh!
Masharti hayo yametolewa na waraka wa wizara ya Mambo ya Nje wa Tarehe 28 Januari 2016 na imeonywa kuwa wale watakaokiuka agizo hilo kuchukuliwa hatua kama walioingilia masuala ya Ndani na siasa za Tanzania.
Woga wote huu ni wa nini? Mlianza kupora ushindi wa Maalim Seif Zanzibar, mkapiga marufuku mikutano ya wagombea walioshindwa, mkafunga magazeti yanayowaeleza ukweli, mkapora uhuru wa Bunge, Mkazuia Televisheni ya Taifa kuonesha Bunge kwa Wananchi na sasa mnajaribu (HASA) kuzuia uhuru wa mawasiliano kati ya taasisi za kiraia na kijamii na Mashirika ya Kimataifa!
Nini kinafichwa na awamu hii? Hofu zote hizi za nini? Je Mabalozi hawa wakiendelea kufanya shughuli zao za uwakilishi na kusikiliza makundi mbalimbali katika nchi si ndiyo moja ya kazi zao? Na mnapoanza kuwadhibiti mnategemea nini? Waje Lumumba kusikiliza ya kwenu tu? Na mbona wale wanaobeba MABANGO ya KIBAGUZI na kupita mbele yenu mkawashangilia hawaombi vibali?
Aibu kubwa kwa taifa! WOGA, UKANDAMIZAJI, U-IMLA......

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top