Vyama 9 vya siasa visiwani Zanzibar vimethibitisha kutoshiriki kwenye uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika Machi 20 mwaka huu kwa kile walichokidai kuwa ni ukiukwaji wa Demokrasia unaoendelea visiwani humo.
Wakiongea leo Jijini Dar es Salaam baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa Zanzibar wamesema kuwa hawakuridhishwa na tume yua uchaguzi Zanzibar ZEC kurudia uchaguzi huo kwani hakukuwa na sababu za msingi za kurudia uchaguzi huo
Hata hivyo licha ya hapo jana rais wa Jamhuri ya muuungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kusema maamuzi ya uchaguzi wa Zanzibar yapo chini ya ZEC wamemuomba rais wa Dkt. Magufuli aingilie kati kukijua kiini cha mgogoro huo kwani chanzo chake si masuala ya kisiasa pekee.
Vyama hivyo vilivyojitoa ni pamoja na DP, CHAUMMA, NRL, JAHAZI ASILIA, DEMOKRASIA MAKINI, SAU, UNDP,UPDP.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment