Umoja wa mataifa umeahirisha mazungumzo ya amani yaliyolenga kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria yaliyodumu kwa miaka mitano.
Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa anayeshughulikia mgogoro huo,Staffan de Mistura amesisitiza kuwa mazungumzo hayo hayajashindikana na yatafanyika tena tarehe 25 mwezi Februari.
Pande zote mbili zimelaumiana kusababisha kusitishwa kwa mazungumzo hayo.
Hatua hii imekuja wakati Serikali ya Syria ikisema imevunja ngome ua upinzani mjini Aleppo.
De Mistura amekiri kuwa jitihada zaidi inapaswa kufanyika
Kiongozi wa ujumbe wa Serikali ya Syria Bashar Jafaar ameshutumu upinzani kusukumwa kwa nguvu ya Saudi Arabia, Qatar na Uturuki na kuchangia kushindikana kwa mazungumzo, televisheni ya taifa nchini Syria imeripoti.
Upinzani nao umeilaumu Serikali na kusema kuwa hawatarejea kwenye mazungumzo mpaka hali itakapoimarika Syria.
Upinzani umeghadhabishwa na kitendo cha vikosi vya serikali ya nchi hiyo kuendelea na mashambulizi mjini Aleppo wakati mazungumzo yakiendelea
MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment