Featured
Loading...

UKIMBEEP CHENGE ATAKUPIGIA TU


Ukiwa msomi uliyebobea katika taaluma fulani na ukakuta kuna mtu anaichezea kada hiyo, ni sawa na mtu ‘kumbeep’ mwenzake tena mwenye vocha, lazima atampigia tu. Kama hujui Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge ni mtaalamu aliyebobea katika masuala ya sheria na hasa za Bunge kutokana na kudumu kwa muda mrefu.
Hata kabla ya kuwa mbunge, Chenge alikuwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye muda wote alikuwa bungeni kwa ajili ya kusimamia masuala ya sheria za nchi na Bunge. Sasa hapa ni sawa na mbuzi kufia kwa muuza supu, Mzee huyo kupewa nafasi hiyo kunaweza kuwa ni msaada mkubwa kwa wabunge wengine na hasa walioingia kwa mara ya kwanza mjengoni.
Leo, Chenge aliacha hiyana na kuamua kumsaidia Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Mngwali baada ya kubaini kuwa alikuwa amevunja kanuni.
Mbunge huyo aliuliza swali la nyongeza, huku akiwa anasoma kwenye karatasi jambo ambalo ni kinyume na kanuni ya 44 ya Bunge na hivyo kumfanya Mwenyekiti Chenge kumpa elimu huku akisema amemsamehe.
Bila shaka mkongwe huyu ataendeleza uzoefu wake wa kumwaga elimu katika Bunge kwa watu wote siyo kwa upande wa upinzani tu.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top