Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkinga Bi. Mboni Mgaza
Hali hiyo inakuja kufuatia baadhi yao kuingia katika hifadhi za misitu na kufanya uharibifu mkubwa wa mazao hayo kisha kusafirisha nchini mwao kwa njia za panya bila kuwa na vibali maalum vinavyotoa mamlaka hiyo.
Akizungumza baada ya ukaguzi uliofanya na kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkinga kukagua uharibifu wa mazao ya misitu unaofanywa na baadhi ya raia wa nchi ya Kenya, Meneja Misitu wilayani Mkinga Bw. Frank Chambo amesema hivi karibuni walitoa taarifa kwa wenzao wa nchi jirani kuwa waheshimu mipaka pamoja na rasilimali za watanzania lakini hatua hiyo haikuweza kufikiwa.
Akielezea jitihada zilizofanywa na serikali katika operesheni inayoendelea hivi sasa ya kudhibiti tatizo hilo,Mwenykeiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkinga Bi. Mboni Mgaza amesema tayari wamekamata bidhaa mbali mbali zitokanazo na mazao ya misitu ikiwemo magunia ya mkaa pamoja na nguzo za miti zikisafirshwa nje ya nchi kinyume cha utaratibu.
Kufuatia hatua hiyo Mwenyekiti wa Wafanyabishara wa nchi jirani ya Kenya Bw. Tito Mayui ameiomba serikali ya tanzania kuimarisha mipaka yake kwa sababu wapo baadhi ya watendaji wake wanazifanyia hujuma fedha ushuru mipakani kwa kisingizio kuwa zinaingia katika maduhuli ya pato la serikali kumbe lakini imebainika kuwa ni kwa ajili ya maslahi yao wenyewe hivyo wameomba serikali kuweka watoza ushuru waaminifu ili waweze kuvuna kisheria na kulipa kodi kwa serikali.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment