Featured
Loading...

Touadera ashinda urais Afrika ya Kati

TouaderaImage copyrightAFP
Image captionTouadera ameahidi kuimarisha usalama
Waziri mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin Touadera ameshinda duru ya pili ya uchaguzi nchini humo.
Matokeo ya awali yanaonesha Bw Touadera alipata karibu 63% ya kura zilizopigwa, na kumshinda mpinzani wake Anicet Dologuele 37% kwenye uchaguzi huo uliofanyika tarehe 12 Februari.
Kwenye kampeni yake Bw Touadera aliangazia sana kurejesha usalama.
Taifa hilo limekubwa na mapigano ya kidini kwa miaka kadha.
Vita vilianza 2013 baada ya waasi wa Kiislamu wa Seleka kuchukua mamlaka.
Bw Touadera, kwenye kampeni yake, alioneshwa na wafuasi wake kama mpenda amani ambaye angeweza kupatanisha Waislamu na Wakristo na kufufua uchumi.
Bw DologueleImage copyright
Image captionBw Dologuele ameahidi kukubali matokeo
Akihutubia wanahabari Jumamosi usiku, Bw Dologuele alisema atakubali matokeo ingawa alisema kulikuwa na kasoro za hapa na pale.
Bw Touadera ameahidi kufanikisha maridhiano na kuhakikisha raia wanasalimisha silaha.
"Uchaguzi huu ni muhimu lakini sio hatua pekee ya kututoa kutoka kwa mgogoro huu. Lazima tuweke mazingira ya kufanikisha mazungumzo kati ya pande zote mbili. Tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaishi pamoja kwa amani.”
Bw Touadera alikuwa profesa katika hesabu na alihudumu kama waziri mkuu chini ya utawala wa Francois Bozize.
Bw Bozize aliongoza miaka 10 hadi serikali yake ilipopinduliwa mwaka 2013 na akatorokea uhamishoni.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top