Spika wa Bunge Mh Job Ndugai amewataka wabunge kuhakisa kuwa waisimamaia vyema serikali katika kutekeleza majukumu yake sanjari na kuhakikisha kuwa bajeti itakayoletwa bungeni kipindi hiki inatekelezeka lengo likiwa ni kuona wananchi wananufaika na serikali yao.
Mh Ndugai ameyasema hayo alipokuwa anafunga mkutano maalum kwa wabunge ambapo amesema ni jukumua la wabunge hoa kujipanga na kuona ni kwa namna gani mambo mengi yatakayoletwa bungeni yanakuwa na manufaa kwa watu wake.
Awali kabla ya kufungwa kwa mkutano huo wabunge walipata nafasi ya kupitia shughuli mbalimbali za kikamati ambapo mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge la katiba na sheria imesema tayari imeielekeza mahakama kukamilisha taratibu za uanzishwaji wa mahakama ya mafisadi.
Naye makamu mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali za mitaa Mh Hilary Aeshi amesema wao katika kamati yao wamejipanga kuhakikisha kuwa maafisa masuhuli wote ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoe sasa hivi wanajirekebisha.
Aidh kamati ya ardhi maliasili na utalii imesema kwa sasa inaelekeza nguvu zake katika kuhakisha kuwa migogoro baiana ya wafugaji na wakulima inapatiwa ufumbuzi kwani kwa muda mrefu sasa watu wamekuwa wakiuwana bila sababu yoyote kama vile hakuna serikali.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment