Serikali imezindua mpango maalum wa kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi ambapo mpango huo unalengo la kupima ardhi nchi nzima na kuwamilikisha.
Akizindua mpango huo waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mh William Lukuvi amesema mpango huo ni mwarobaini wa migogoro ya mara kwa mara baina ya wakulima na wafugaji lakini pia kwa watu wengine na hasa wale matapeli wa ardhi.
Naye mratibu wa mpango huo Bw Godfrey Machabe amesema wananza na mkoa wa Morogoro ambao unamigogoro mingi baina ya wakulma na wafugaji.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Rajabu Rutengwe amesema mpango huo utasaidia kuondoa migogoro na kuwapa wananchi fursa ya kumiliki ardhi ambayo wataweza kwenda benki kuchukua mikopo na kuinuka kiuchumi
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment