Featured
Loading...

Serikali ya SMZ yawataka polisi visiwani Pemba kusimamia vyema uchaguzi wa marudio.


Naibu waziri wa mambo ya ndani ya Mh Hamad Yusuf Masauni amewataka askari polisi mkoa wa kaskazini Pemba kujitahidi  kusimamia ipasavyo uchaguzi wa marudio ujao ili kuhakikisha  unafanyika katika hali ya utulivu na amani.
 
Mh Masauni ametoa wito huo kwenye ukumbi wa polisi mkoa wa kaskazini Pemba alipokua akizungumza na maafisa na askari wa mkoa  wa kaskazini Pemba.
 
Mapema Mh Masauni alitembelea nyumba  wanazokaa askari polisi laini  wete na baadae kukagua ujenzi wa nyumba ya kufikia wageni FFU Finya  ambayo inaendelea na ujenzi na kuelezwa kuwa inahitaji zaidi ya  shilling million 40 hadi kumalizika kwake.
 
Akisoma taarifa fupi ya ujenzi huo kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini Pemba Hassan Nassir Ali amesema hadi hatua uliofikia ujenzi  huo zaidi ya shilling million 20 tayari zimeshatumika.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top