Baadhi ya Viongozi waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Sheria wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa. Kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa Kenya Dkt. Willy Mutunga, Jaji Kiongozi wa Tanzania Mhe. Shaaban Lila (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Mecki Sadiki.
Baadhi ya Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini na wadau muhimu wa Mahakama waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Sheria wakitoa heshima zao wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Charles Rwechungura akitoa salam na ujumbe wa Chama hicho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia) akifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga.
Jaji Mkuu wa Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwahutubia viongozi, mabalozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kuhusu utendaji wa Mahakama na Utoaji wa Haki kwa wananchi kwa wakati kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria. Mhe. Rais alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na viongozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama ya Tanzania leo wakati wa kilele cha Siku ya Sheria nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini na baadhi ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania wakati wa kilele cha Siku ya Sheria.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mawakili.
Jaji Mkuu wa Kenya Dkt. Willy Mutunga (kulia) akimkabidhi zawadi ya kumbukumbu kutoka nchini Kenya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo jijini Dar es salaam. Jaji Mkuu wa Kenya alikua miongoni mwa wageni mashuhuri walioalikwa na Mahakama ya Tanzania kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria.
Wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria wakifurahia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli aliyokua akiitoa leo jijini Dar es salaam.
MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment