SWALI GUMU KIDOGO
Siku moja baada ya kuamka asubuhi ghafla kupitia dirishani nilimuona ndege akiwa ametua juu ya tawi la mti. Nikakumbuka ule msemo usemao kwamba ndege wa angani hawana mawazo wala matatizo kama binadamu.
Lakini katika maisha unaweza kumuona mtu usiyemjua akiwa katika shughuli zake akifanya matumizi makubwa au akitembelea magari la gharama au mtu mwenye wadhfa mkubwa na jamii inamuita tajiri na yeye akionekana mwenye furaha lakini ukichukua muda wa kuwa rafiki yake na kutembea nae katika maisha yake utagundua kwamba mtu huyo ni kama wengine ana matatizo na mawazo
Kisha nikarudi kujiuliza tena swali ...Je ni kweli kwamba ndege hawana mawazo/matatizo au ni kwa kuwa hatujatembea nao na kuona wanapopita au shida wanazozipata?
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment