Mgomo wa madereva wa daladala jijini Mbeya umeingia katika siku ya pili na kusababisha adha kubwa ya usafiri kwa wakazi wa jiji ambao baadhi yao wameshindwa kuelekea katika maeneo yao ya kazi za kila siku.
Licha ya serikali kusikiliza madai ya madereva wa daladala katika halmashauri ya jiji la Mbeya na kuamua kuwabadilishia njia za kupita, bado madereva hao wameendelea na mgomo wao wakitaka barabara mpya walizopangiwa kupita zifanyiwe marekebisho.
Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Dk. Samwel Razalo amesema kuwa malalamiko ya madereva hao kuhusu ubovu wa barabara yamefanyiwa kazi kwa kuwabadilishia njia kwa muda ili kupisha matengenezo ya barabara hizo ambayo yataanza baada ya msimu wa mvua kumalizika hivyo hawana sababu za kuendelea na mgomo wao.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Mbeya, wameunga mkono mgomo huo wa madereva huku wakiitaka serikali kushughulikia tatizo la madereva hao haraka ili kurejesha hali ya usafiri kama kawaida.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment