Lukuvi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akikabidhi ramani za maeneo ya mitaa yote ya jiji kwa watendaji na wenyeviti wa mitaa ili kila mwananchi ajitambue eneo alilojenga kama hakustahili kuwepo aanze kujipanga.
Baadhi ya mameya waliohudhuria makabidhiano hayo mbali na kuelezea mipango ya manispaa zao juu ya suala la mipango miji wamesema baada ya wizara kutoa ramani hizo tatizo sugu la migogoro ya ardhi litapungua kwani kila mmoja atafuata taratibu na sheria zilizopo.
Wilaya ya Kinondoni ni miongoni mwa wilaya zinazodaiwa kuongoza kwa kuwa na migogoro mingi ya ardhi ambapo afisa mipango miji Bi Juliana Letara amesema asilimia 70 ya maeneo bado hayajapimwa wala kurasimishwa hali inayochangia manispaa hiyo kukosa mapato. MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment