Spika wa bunge Mh Job Ndugai amesema bunge litaendelea kudumisha mahusiano yaliyopo kati ya bunge la Sweden na Tanzania kutokana na manufaa ambayo nchi imeyapata ikiwemo nyanja ya elimu, afya na teknolojia ya gesi.
Mh Ndugai ameyasema hayo ofisi ndogo ya bunge jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na baadhi ya wabunge kutoka bunge la Sweden ambao wamekuja nchini kufuatilia namna nchi inavyotekeleza shughuli za maendeleo.
Naye balozi wa Sweden hapa nchini ambaye ameambatana na wabunge hao Bi Katharina Rangnitt amesema yapo mambo mengi ambayo nchi yake inajifunza kupitia bunge la Tanzania hivyo wataendelea kuimarisha uhusiano huo hasa katika nyanja ya kiuchumi.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment