Zaidi ya askari mgambo 50 waliosimamia mtihani wa kidato cha nne Novemba 2 mwaka jana katika shule 47 za sekondari za halmashauri ya manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wamevamia ofisi ya mkurugenzi wa manispaa hiyo wakishinikiza kulipwa madai yao zaidi ya shilingi milioni 30, huku polisi waliokuwa na silaha za moto pamoja na mabomu ya machozi wakilazimika kuwatawanya ili kuimarisha ulinzi katika ofisi hizo.
Askari mgambo hao wakiwa wamevalia kombati zao, walianza kuwasili katika ofisi za halmashauri ya manispaa ya Ilemela kuanzia majira ya saa moja asubuhi, wakiwa na matumaini ya kulipwa madai yao ambayo wamekuwa wakiahidiwa kila mara na mkurugenzi wa manispaa hiyo John Wanga, lakini walijikuta matumaini yao yakiyeyuka ghafla mithili ya umande wa alfajiri ilipofika majira ya saa kumi na moja na nusu jioni baada ya kuitiwa askari polisi waliokuwa na silaha za moto na mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatawanya.
Afisa habari wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela Viola Mbakile akizungumza na ITV kwa njia ya simu kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa hiyo amesema askari mgambo hao na baadhi ya askari polisi waliosimamia mtihani huo wa kidato cha nne kwa muda wa wiki tatu kuanzia tarehe 2 hadi 27 Novemba mwaka jana, watalipwa stahiki zao Jumamosi Februari 6 na kila mmoja anatakiwa kwenda na kitambulisho chake, huku afisa elimu sekondari Juma Kasandiko akipata kigugumizi cha kueleza sababu zilizomfanya kuwaita askari polisi ili kuwatawanya baadhi ya askari mgambo hao walioamua kupiga kambi katika ofisi za manispaa hiyo.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment