Featured
Loading...

Al-Shabab wasema ndio walioshambulia ndege

NdegeImage copyrightHarun Maruf
Image captionNdege hiyo ilitoboka shimo ikiwa angani
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al-Shabab kutoka Somalia limesema ndilo lililoshambulia ndege iliyotoboka shimo ikiwa angani mapema mwezi huu.
Kupitia taarifa iliyotumwa kwa barua pepe al-Shabab wamesema shambulio hilo lilikuwa la kulipiza kisasi operesheni za kijasusi zinazoendeshwa na mataifa ya Magharibi nchini Somalia.
Shimo hilo kwenye ndege hiyo lilitoboka muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka Mogadishu, ikiwa futi 10,000 (3,048m) juu angani.
Ndege hiyo ilifanikiwa kutua kwa dharura.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Daallo, iliyokuwa ikielekea Djibouti, ilikuwa imebeba watu karibu 60.
Maafisa nchini Somalia baadaye walitoa video inayoonesha watu wawiliwakimkabidhi abiria mmoja anayeshukiwa kuwa mlipuaji wa kujitolea mhanga kitu kinachoonekana kama Laptop kabla ya mlipuaji kuabiri ndege hiyo.
Msemaji wa serikali anasema kuwa watu hao ndio washukiwa wakuu katika ulipuaji huo.
Inasadikika kuwa mmoja kati ya watu walioleta kipakatilishi hicho alikuwa ni mfanyikazi wa shirika linalohudumu katika uwanja huo wa ndege wa Mogadishu.
Watu 20 wamekamatwa wakiwemo wale wawili walionaswa kwenye video hiyo.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top