Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imefuta kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi katika Jimbo la Ilemela, yaliyompa ushindi Angelina Mabula wa CCM, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Kesi hiyo ilifutwa baada ya mlalamikaji aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo wa Chadema, Highnes Kiwia kushindwa kulipia Sh10 milioni ili kuanza kusikilizwa baada ya kufunguliwa Novemba 25, mwaka jana.
Kiwia alifungua kesi hiyo akidai kuwa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana hakuwa huru na haki kwa sababu baadhi ya vituo katika jimbo hilo majina ya wapigakura yaliongezwa na mawakala wake kutishiwa na baadhi ya wafuasi wa CCM.
Akitoa uamuzi wa kufuta kesi hiyo jana saa 3:00 asubuhi, Msajili wa Mahakama Kuu wa Kanda hiyo, Eugenia Rujwahuka alisema Mahakama hiyo imekubaliana na hati iliyowasilishwa na Wakili wa kujitegemea ambaye alikuwa akimtetea Kiwia, Paul Kipeja
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment