Featured
Loading...

STAND UNITED SASA MAMBO POA, NI BAADA YA WAZIRI WA MICHEZO KUTUMBUA MAJIPU


Stand UTD-Benchi la ufundi
Mwenyekiti wa klabu ya Stand United ya Shinyanga Amani Vincent amewataka wadau, wanachama na viongozi wote wa klabu hiyo kuungana na kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha timu yao inasonga mbele baada ya kutoka mikononi mwa wavamizi.
Klabu ya Stand United iliingia kwenye mgogoro mara baada ya klabu hiyo kupata udhamini kutoka kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA.
Baada ya Stand kupata udhamini, iliundwa timu maalumu ya uboreshaji wa Stasnd United chini ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally N. Rufunga.


Mara baada ya Mh. Nape Nauye kuteuliwa kuwa Waziri mwenye dhamana ya kusimamia michezo, uongozi wa Stand United ulimfuata Mh. Nnauye na kumweleza kila kitu juu ya namna timu yao ilivyovamiwa na ‘maharamia’ kufutia kupata udhamini kutoka ACACIA.Barua ya kusitisha uteuzi wa kuwa mweka hazina wa timu maalumu ya uboreshaji wa Stand United FC

Barua ya kusitisha uteuzi wa kuwa mweka hazina wa timu maalumu ya uboreshaji wa Stand United FC
Nape Nnauye kama Waziri mwenye dhamana ya kusimamia michezo, aliwaomba wale wote ambao wanalalamikiwa kuivamia Stand United waiache mikononi mwa uongozi uliopambana kuifanya klabu hiyo ipate udhamini.
Tayari mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mh. Ally N. Rufunga amewaandikia barua za kusitisha uteuzi wa viongozi wote walioteuliwa kwenye kamati hiyo ambayo ilipewa jina la uboreshaji wa Stand United FC.
Mwenyekiti wa Stand Uinted amewataka wadau wote kuipa support timu yao baada ya kurudishwa mikononi mwao na kuwataka waachane na mambo ambayo yamepita bali waangalie katika kuijenga timu yao na kuhakikisha inasonga mbele.
Barua ya kusitisha uteuzi wa kuwa Katibu wa timu maalumu ya uboreshaji wa Stand United FC
Hili ni jambo ambalo tulikuwa tunaliomba muda mrefu ili tuweze kupata nguvu kwenye kamati yetu ya utendaji, mimi nafikiri kutokana na suala hili kuwa limefanikiwa linatupa changamoto sisi kufanya kazi ya kuuthibitishia umma kwamba tunaweza kufanya kazi.
Lakini isitafsirike kitu chochote kama labda kuna mshindi juu ya jambo hili, baada ya hili naomba support kwa wadau, wanachama na wapenzi wa soka ili tuendeleze mpira wetu na tuendelee kufanya kazi kama ilivyokuwa hapo awali.

Yule ni kiongozi wa serikali, mimi natumia fursa hii kuwaambia wajumbe wa kamati ya utendaji, wanachama na wadau wengine, kutokana na suala hili kumalizika kwa yeye kuondoa kamati yake, nisingependa kusikia tena viongozi wa klabu au  mtu yeyote anayetoka klabu ya Stand anazungumza jina la mkuu wa mkoa kwenye vyombo vya habari.
Barua ya kusitisha uteuzi wa kuwa makamu mwenyekiti wa timu maalumu ya uboreshaji wa Stand United FC
Barua ya kusitisha uteuzi wa kuwa Katibu wa timu maalumu ya uboreshaji wa Stand United FC
Kwasasa inabidi tuwe kawaida, tukubali kuwa yale yaliyotokea yamekwisha tufanye kazi ya mpira kwasababu vinginevyo tutaathiri matokeo mengine au tutaanza kupata njama zingine za kutaka kuanza kuhujumiana. Sisi tutatoa fursa pana bahati nzuri Waziri Nape Nnauye alisema kwamba tuajiri wataamu na tuwe na secretariat nzuri ili mkataba usimamiwe vizuri.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright 2025 UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top