Featured
Loading...

Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa Chapigwa Faini Ya Milioni 50


Serikali imetoa siku saba kwa kiwanda cha sukari cha Mtibwa kulipa faini ya shilingi milioni 50 baada ya kudaiwa kukiuka sheria za mazingira.

Baadhiya mambo yaliyobainika ni kukosa mfumo mzuri wa kuhifadhi na kusafirisha taka ngumu na taka maji, kutohifadhi vyema kemikali zinazotumiwa na kiwanda hicho pamoja na kutumia kuni kuendesha baadhi ya mitambo yake hususani eneo la kuchemshia.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya kufanywa kwa ziara ya kushtukiza kiwandani hapo na naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Luhaga Mpina, aliyeambatana na wataalamu kutoka baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC).

Mh Mpina amesema tayari serikali ilishakataza viwanda kutumia kuni na magogo kuendeshea mitambo yake, huku akitoa siku 30 kwa uongozi wa kiwanda hicho cha Mtibwa kufanyia marekebisho mapungufu yote yaliyotajwa vinginevyo serikali itakifunga.

Akiwa kiwandani hapo naibu waziri Mpina amewaagiza viongozi wa mamlaka mbalimbali kuwajibika katika agizo la usafi wa mazingira kwa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi sambamba na kuwaagiza wakurugenzi wa halmashauri za wilaya kuhakikisha miti milioni 1.5 inapandwa kila mwaka.

Kaimu meneja mkuu wa kiwanda cha sukari Mtibwa Ahmad Yahya pamoja na kuridhia maagizo yaliyotolewa, ameiomba serikali kuwapunguzia faini hiyo ya shilingi milioni 50 ambayo amedai kuwa ni nyingi kwa kiwanda hicho kumudu

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top