Featured
Loading...

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda akamatwa

Image captionJenerali mstaafu David Sejusa amekamatwa majuma 3 kabla ya uchaguzi
Mwanasiasa maarufu wa Uganda, Jenerali David Sejusa, amekamatwa, wiki tatu hivi kabla ya uchaguzi mkuu.
Wakili wake amesema askari jeshi waliizunguka nyumba yake leo alfajiri.
Inaarifiwa kuwa amewekwa katika kifungo cha nyumbani.
Jenerali Sejusa alikuwa mshirika wa karibu wa Rais Yoweri Museveni, ambaye ameongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30, anagombea uongozi tena katika uchaguzi wa tarehe 18 Februari.
Jenerali Sejusa, alikimbilia nchi za nje miaka mitatu iliyopita, baada ya kumshutumu rais Museveni, kuwa alikuwa akimuanda kimyakimya mwanawe kurithi uongozi.
Hii sio mara ya kwanza kwa mwanasiasa huyo kukamatwa, tangu kurudi Uganda.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright 2025 UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top