somalia
lililotegwa ndani ya gari limelipuka nje ya mgahawa mmoja uliopo katika ufukwe wa bahari katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu,kulingana na maafisa wa polisi.
Walioshuhudia wamemwelezea mwandishi wa BBC Ibrahim Aden kwamba gari hilo lililojaa vilipuzi liligonga mgahawa huo maarufu wa Lido Beach kabla ya watu watano kujitokeza na kuanza kufyatua risasi.
Haijulikani iwapo kumekuwa na majeruhi.
Hakuna kundi lililokiri kutekeleza shambulizi hilo,lakini kundi la Alshabaab ndilo linaloshukiwa kwa kutekeleza mashambulizi mengine kama hayo hapo awali.
Ufukwe wa bahari nchini Somalia
Mgahawa wa Lido Beach uliopo pembezoni mwa Mogadishu,huwavutia maelfu ya vijana wa Somalia wanaojifurahisha.
Migahawa kadhaa imefunguliwa katika ufukwe huo katika miaka ya hivi karibuni.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Meja Abdiqadir Ali amekiambia chombo cha habari cha reuters kwamba shambulio hilo lilitokea katika lango la mgahawa huo.
Amesema kuwa uchunguzi unaendelea.
MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment