#pichani_Ujenzi wa nyumba za muda kwa familia za wahanga wa tukio la mauaji ya watu nane kuchinjwa kijiji cha Kibatini kata ya Mzizima Amboni Tanga na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi ukiendelea kijiji cha Kona Zedi kata ya Kiomoni Tanga.
#pichani_Mhanga wa tukio la mauaji kijiji cha Kibatini kata ya Mzizima Amboni Tanga, Mrahagwa Magwe (75) akiwa uwanjani kijiji cha Kona Zedi kata ya Kiomoni Tanga alikokimbilia baada ya kuyahama makazi yao, Mzee huyo kwa sasa analala nje usiku mchana mvua jua na kutojua hatma yake na vifaa vyake vya ndani.
Kwa sasa mzee huyo wa makamo anaishi uwanjani kulinda thamani zake ikiwemo vitanda na magodoro ambayo nyakati za mvua zimekuwa zikinyeshewa na mvua. Mzee huyo analalamika nyakati za usiku kupigwa na baridi kali hivyo kuwaomba wasamaria wema kumsaidia kwa lolote ili kuweza kujisitiri.
Mzee huyo amekuwa akishinda katika vyombo vyake ili kuepuka kuibiwa au kuharibika na wapita njia.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment