Benki kuu ya Nigeria itaruhusu sarafu yake kushuka thamani kuanzia juma lijalo.
Akihutubia kwa njia ya televisheni, Gavanna wa benki kuu Godwin Emefiele amesema, thamani ya kubadilisha fedha itakuwa ikidhibitiwa
Tangu mwezi wa Februari mwaka jana thamani ya ubadilishaji fedha ilikua ni kiasi cha naira 197 kwa dola moja ya marekani na katika masoko yasiyo rasmi gharama yake inafika mpaka karibu na Naira 350.
Hatua hiyo inakusudia kupambana na changamoto ya kukosekana kwa fedha za kigeni,kulikosababishwa na kuanguka kwa bei ya mafuta na kuvutia wawekezaji.
Lakini mwandishi wa BBC jijini Lagos anasema hali hii inaweza kusababisha kupanda kwa gharama za bidhaa na kusababisha athari kubwa kwa mamilioni ya Raia wa Nigeria wanaoishi kwenye lindi la umasikini.
MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment