Kutokana na kukithiri kwa tabia za waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda na abiria wao kutovaa helmet kichwani (kofia maalum ngumu) wakati wa safari, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kuwakamata na kuwafungulia mashtaka.
Makonda alisema kuwa watu wanaotumia usafiri huo bila kuvaa helmet kichwani wanafanya kosa sawa na kutaka kujiua, hivyo watashtakiwa.
“Nimeshawasiliana na kamati yangu ya usalama barabarani mkoa, hili nitalisimamia kikamilifu lazima wote wawe na helmet na wakikamatwa wote watashtakiwa,” alisema Makonda.
Alifafanua kuwa kutovaa kofia hiyo maalum wakati umepanda usafiri huo, ni sawa na mtu anayetaka kujiua kwa kunywa vidonge na pombe kali.
Makonda alisisitiza kuwa atalisimamia kwa nguvu zoezi hilo hususan katika kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili aweze kupata dhawabu kwa Mungu kwa kuokoa maisha.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment