Soko jipya la Mwanjelwa kwa muonekano wa ndani
Soko hilo lililokamikilika hivi karibuni kwa gharama ya shilingi bilioni bilioni 5.3 limesusiwa na wafanyabiashara hao ambao wameelezea kiwango cha kodi ya shilingi laki tano walichopangiwa na halmashauri ya jiji kwa mwezi ni kikubwa tofauti na mitaji yao.
Wafanyabaishara hao leo wamelazimika kusitisha shughuli ya uchaguzi wa viongozi uliopangwa kufanyika kwa mujibu wa katiba yao na kumtaka kaimu mkurugenzi wa jiji la Mbeya Vicent Msolla kuondoka na kero hiyo na kwenda kuifanyia kazi.
Kaimu mkurugenzi wa jiji la Mbeya Vicenti Msolla amekiri kuwa lengo la serikali lilikuwa ni kutoa kipaumbele kwa ajili ya wahanga wa ajali ya moto mwaka 2006 lakini gharama za ujenzi wa soko zilizotumika ni kubwa ndiyo maana halmsahauri imependekeza kodi hiyo.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment