Featured
Loading...

CCM Kigoma yawafukuza wanachama 25 kwa kuwasaliti kipindi cha Uchaguzi

Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Kigoma kimewafukuza uanachama 25 wa chama hicho baada ya kukisaliti chama kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Okt0ba 25 Mwaka jana.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwenye ukumbi wa CCM Mkoa Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala alisema kuwa uamuzi huo wa kuwafuata uanachama ulitolewa na kikao cha halmashauri kuu cha Mkoa kilichofanyika tarehe 2 march mwaka huu.

Naomi alisema kuwa baaada ya uchaguzi mkuu kufanyika chama kilianza kufanyatathimini na changamoto walizokutana nazo kipinchi cha uchaguzi mkuu.

''Kwenye tathimini yetu hiyo tuliweza kugundua kuna baadhi ya wanachama ambao walikuwa siyo waaminifu kipindi cha uchaguzi mkuu walikuwa wakikisaliti chama tena wengine walikuwa viongozi na wengine waliogombea ubunge na kushindwa kwenye kura za maoni tumeamua watupishe sisi tuendelee kutekeleza ilani ya chama''alisema Kapambala.

Aliwataja wanachama waliofukuzwa uanachama kuwa ni pamoja Venance Mpologomi,Paul bahinda, Damasi Shetei,Gidioni Bunyanga,Edger Mkosamali,Pili Waziri,Pendo Jumanne,Robinson Lembo na Juma matete.

Wengine waliofukuzwa uanachama ni Idd Lugundanya,Juma Kifuku,Edga Bisoma,Staphord Kumuhanda,Jenoveva Bisana,Salehe Anatori,Abdallah Chugu,Atanas Andrea,Bigilimana Vyanda,Jonas Kafyiri,Isack Braytony,Christopher Chiza,Fanuel Kasogota,Laulent Bikulamuchi,Ibramu Shikuzilya na Paul Chabandi.

Alisema wanachama hao walifukuzwa uanachama wa chama cha mapinduzi tayari wameshahamia vyama vingine pia tathimini ya uchaguzi Mkuu bado inaendelea.

Naye Katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Kigoma Staney Mkandawile alisema kuwa sasa hivi kazi iliyopo ni kutekeleza ilani ya chama na kuumunga mkono Rais John Magufuli kauli mbiu ya hapa kazi tu.

''Chama hakitamuonea mtu yeyote,ni bora tubaki wachache ndani ya chama lakini tuwe tunatekeleza ilani ya chama na kukipenda chama"Alisema Mkandawile

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top