Featured
Loading...

Zitto Kabwe

Wanafunzi 1941 walitahiniwa katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2015 katika Jimbo langu ( Manispaa ya Kigoma Ujiji) lenye jumla ya Shule za Umma 18. Matokeo yao ni kwamba 86% wamepata daraja la nne na sifuri na 14% tu Ndio wamepata madaraja la kwanza mpaka la Tatu.
Watahiniwa 21 wamepata Daraja la Kwanza, 83 Daraja la Pili, 194 Daraja la Tatu, 806 Daraja la Nne na 837 Sifuri. Tupo chini ya Wastani wa Kitaifa!
Ni matokeo mabaya sana. Kama Mbunge wa Jimbo hili 2015 - 2020 ni wajibu wangu kuhakikisha kuwa tunaongeza ufaulu na kukata idadi ya sifuri kwa kiwango kikubwa kama sio kutokomeza kabisa. Msingi wowote wa Elimu ni elimu ya msingi, nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuboresha elimu ya Msingi kama mkakati endelevu na kupandisha ufaulu Kuanzia mwaka huu kama mkakati wa muda mfupi na muda wa kati.
Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kigoma Ujiji litaunda kikosi kazi cha walimu wastaafu na wadau wa Elimu kuandaa mkakati wa Elimu wa Manispaa. Sisi hatuna 'luxury' ya kulaumiana na kutafutana mchawi. Acha tutafute majawabu ya Changamoto zetu. Manispaa ya Kigoma Ujiji chini ya ACT Wazalendo ina dhamira ya kuwa Manispaa ya mfano katika kuondoa aibu tuipatayo kwenye Elimu.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top