Featured
Loading...

Wananchi waomba matengenezo ya dharura ya barabara ya Mpanda kuwaondolea adha ya usafiri.

Kufungwa kwa barabara ya Mpanda mkoani Katavi hadi Tabora yenye urefu wa zaidi ya kilomita 360, kufuatia daraja la mto Koga kusombwa na maji ya mafuriko, kumesababisha adha kubwa kwa wananchi wanaotumia usafiri wa kwenda Tabora na mikoa mingine ya kanda ya ziwa, pamoja na maeneo ya kaskazini mwa nchi, na hivyo kuiomba serikali ifanye matengenezo ya dharura ili kuwaondoa kwenye adha hiyo.
 
Wakiongea na ITV kwenye maeneo ya kituo kikuu cha mabasi cha mjini Mpanda, ambacho kimekuwa kitupu isivyo kawaida kwa sasa kufuatia makampuni mengi kusimamisha usafiri, baadhi ya wananchi wamesema hivi sasa wakitaka kusafiri kwenda Tabora, Mwanza, Arusha na maeneo mengine, inabidi wazungukie uvinza mkoani Kigoma, ambako licha ya kurefusha safari lakini pia hata gharama za usafiri zimeongezeka mno.
 
Nao baadhi ya mawakala wa usafirishaji katika kituo hicho kikuu cha mabasi cha mjini Mpanda, wameeleza kuwa hali ya kibiashara hivi sasa imekuwa ngumu kufuatia abiria kupungua mno kwa ajili ya ugumu wa safari, kwani hata abiria waliokuwa wakitoka Sumbawanga mkoani Rukwa wakitaka kupitia Mpanda kwenda Tabora hadi Mwanza, wameacha kutumia njia hiyo kuepukana na adha iliyopo.
 
Wakitembelea kushuhudia athari ya mafuriko hayo yaliyosomba daraja la mto Koga, baadhi ya viongozi wa mkoa wa Katavi akiwemo mkuu wa mkoa huo, waliamua barabara hiyo ifungwe ili isije ikaleta madhara makubwa ikiwa ni pamoja na vifo.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top