Featured
Loading...

Wanafunzi SUA walia na bodi ya mikopo.

Wanafunzi 204 wakozi tofauti katika chuo kikuu cha sokoine cha kilimo SUA wako hatarini kushindwa kuendelea na masomo kufuatia bodi ya mikopo kushindwa kuliwapa feha za mikopo kwa madai kuwa hawajapeleka vielelezo vyao  licha ya serikali ya wanafunzi kuwasilisha vielelezo hivyo  hali inayosababisha wanafunzi hao kuishi kwa tabu chuoni.
Akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho Osca Ndunguru ametupia lawama bodi ya mikopo kuendelea kuwatesa wanafunzi huku wanafunzi hivyo amemuomba rais Magufuli kutembelea bodi ya mikopo  kuchunguza uozo unaofanyika  na kwamba bodi hiyo ihakikishe inashugulikia tatizo la wanafunzi hao ndani ya siku tatu.
 
Nao baadhi ya wanafunzi walioathiriwa na tatizo la kukosa mikopo wameeleza kusikitishwa kwao na kwamba wanalazimika kuishi kwa tabu kwa kukopeshana wanafunzi kwa wanafunzi wakitegemea bodi ya mikopo itawalipa fedha zao lakini kadri siku zinavyozidi kusonga mbele hali ya maisha yao chuoni yanazidi kuwa magumu.
 
Waziri mkuu wa serikali hiyo ya wanafunzi amesisitiza na kuiomba serikali ya rais Magufuli kuangalia upya mfumo wa utendaji wa watumishi wa bodi ya mikopo kwani wanafanya kazi hiyo kwa mazoea na upendeleo kwa baadhi ya watu hali inayozorotesha maendeleo ya nchi.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top