Baada ya malalamiko ya wabunge wa upinzani juu ya wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge, Spika wa Bunge, Job Ndugai, anatarajia kuzipangua kamati hizo.
Taarifa za uhakika toka Bungeni mjini Dodoma zinasema, licha ya kuwapo kwa baadhi ya wajumbe walioomba kuhamishwa kwenye kamati walizopangiwa awali, kumekuwapo na mazungumzo kati ya Kambi ya Upinzani Bungeni na kiti ofisi ya Spika juu ya suala hilo.
Inaelezwa kati ya wajumbe watakaohamishwa kutoka kwenye kamati zao za awali ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe aliyekuwa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Jamii na sasa atapelekwa Hesabu za Serikali (PAC).
Naye Mbatia aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Miundombinu, sasa atapelekwa kwenye Kamati ya Bajeti aliyokuwa akitumikia kwenye Bunge la 10.
Spika wa Bunge, alipotafutwa ili kuzungumzia suala hilo kupatikana.
Juzi Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bunge, Tundu Lissu, alisema wanafikiria kumpeleka Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, kwenye kamati ya PAC ili awe mwenyekiti wao.
“Wasipokubali (kubadilisha wajumbe) hatutakubali ungozi tutaacha, mimi mwenyewe sheria ndogo siendi, huko ni kupoteza muda kwa sababu hakuna kamati ya ovyo vile, nitaenda sheria na katiba na kushiriki mijadala, kura tu ndiyo sintopiga, hoja yoyote ya kisheria ikiibuka bungeni nitaibuka na watashangaa,” alisema Lissu.
MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment