Simba wasiojulikana idadi yao wametoroka mbuga ya taifa ya wanyamapori ya Nairobi. Taarifa zinasema mara ya mwisho walionekana eneo la makazi la Langata.
Tayari shirika la wanyama pori la Kenya KWS limeanzisha oparesheni ya kuwasaka wanyama hao.
Shirika hilo limewataka wakaazi wa maeneo hayo kutahadhari.
Hii si mara ya kwanza kwa wanyama hao kuzua taharuki katika eneo hilo.
Msemaji wa Shirika hilo Paul Udoto ameambia BBC nchini Kenya kwamba wamepokea habari kwamba simba hao wa kike walionekana katika nyumba za NHC katika eneo la Langata na mitaa mengine inayopakana na Barabara ya kusini.
''Haya ni maeneo ambayo yana watu wengi,na hii ndio maana tumeimarisha msako wetu,'' aliambia BBC kwa njia ya simu, yeyote aliye na habari kuwahusu anapaswa kutoa habari hizo mara moja.
''Kikosi chetu kikishirikiana na madaktari wa wanyama kimeenda eneo la Langata kuwasaka wanyama hao tangu saa kumi na moja asubuhi,'' aliongezea.
Langata ni eneo lililo na watu wengi na maafisa wa KWS pamoja na polisi wanahofia kwamba wanyama hao huenda wakasababisha hasara iwapo hawatapatikana haraka na kurudishwa katika mbuga hiyo.
Simba sita waliripotiwa kutoroka katika mbuga hiyo Alhamisi jioni lakini wanne kati yao walipatikana .
MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment