Serikali imewaagiza wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote nchini kuchukua hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi watumishi wa idara ya ardhi ambao wamebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa hatua ambayo imetajwa kuchangia migogoro mingi ya ardhi katika maeneo yao.
Agizo hilo limetolewa mjini musoma na naibu waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh Angelina Mabula, wakati akizungumza katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali za wizara yake mkoani Mara, ambapo amesema serikali imebaini kuwa migogoro mingi ya ardhi imechangiwa kwa kiasi kikubwa watumishi wa idara hiyo kwa maslahi binafsi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bunda Bw Joshua Mirumbe, amewataka wananchi wote ambao tayari wamelipwa fidia kwa ajili ya kupisha eneo uwekezaji wa kiuchumi EPZ kuondoka mara moja kabla ya serikali haijachukua hatua za kuzivunja nyumba hizo, huku katibu tawala wa mkoa wa Mara Bw Benedict Ole Kuyani akiomba serikali kutoa fedha za uendeshaji wa mabaraza ya ardhi hatua ambayo amesema itasadia kutatua migogori mingi ya ardhi mkoani Mara.
Naye kamishina wa ardhi kanda ya ziwa Bw Joseph Shewiyo, akizungumza katika kikao hicho ambacho kimeshirikisha viongozi na watendaji wa halmashauri za mkoa wa Mara, ameagiza halmashauri zote kusimamia sheria kwa kubomoa nyumba zote ambazo zimejengwa baada ya mwezi mei mwaka 2001 ndani ya mita sitini katika maeneo ya fukwe za ziwa, mito, maneo ya wazi na hifadhi za barabara.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment