Siku moja baada ya klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji imsajili mshambuliaji wa kimataifa waTanzania aliyekuwa anaichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia yaKongo Mbwana Samatta, January 30 ilishuka dimbani ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani Cristal Arena kuikabili klabu ya Kortrijk.
Licha ya kuwa Samatta hakuwa kwenye kikosi, kwa sababu hakufanya mazoezi na timu,KRC Genk imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na mshambuliaji mwenye asili ya Zaire Christian Kabasele dakika ya 21, hizi ni taarifa na mapokezi mema kwa Samatta ambaye ndio kwanza ametua Ubelgiji kuanza maisha yake ya soka.
Mchezo wa mwisho kabla ya ushindi dhidi ya Kortrijk, KRC Genk ilicheza dhidi yaMechelen na kutoka sare ya goli 1-1, kwa sasa KRC Genk ipo nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi. KRC Genk watarudi uwanjani February 6 kucheza dhidi ya Mouscron-Peruwelz na huenda mchezo huo Mbwana Samatta akawepo.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment