Featured
Loading...

Mfanyakazi wa Tanesco wilayani kilosa apata kichapo kutoka kwa wananchi.

Wananchi wa kijiji cha Lumuma wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wameandamana kwa kufunga barabara na kumpiga mfanyakazi wa shirika la ugavi wa umeme Tanesco wakilalamikia shirika hilo kupitisha nguzo za umeme kwenye mashamba yao kupeleka nishati hiyo katika vijiji jirani bila wao kupatiwa huduma hiyo.
Wakizungumza kijijini hapo wananchi hao wamesema wameamua kuandamana na kufunga barabara kufuataia shirika la umeme Tanesco kushindwa kusambaza huduma hiyo katika kijiji hicho na badala yake kupitisha nguzo katika maeneo yao kupeleka huduma katika vijiji vya jirani ambapo wamesema hawapotayari kuruhusu mradi huo kuendelea hadi watakapohakikishiwa kuunganishiwa nishati hiyo. 
 
Nao viongogozi wa kata na kijiji cha Lumuma wamesema wanaunga mkono wananchi kwani wamesema inaonekana zoezi hilo limegubikwa  na hujuma huku wameomba serikali na uongozi wa Tanesco kuona uwezekano wa kuanza kusambaza umeme katika kijiji cha Lumuma na badaye kumalizia katika vijiji vilivyoko katika kata hiyo.
 
Akiongea na ITV kwa  njia ya simu meneja Tanesco mkoa wa Morogpro Mhandisi John Bandiye amesema anatambua kuwepo mradi wa umeme katika kata ya Lumemo lakini hafahamu kama wananchi wa kijiji hicho wanalalamika na kwamba atafuatilia ili kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top